Swali: Ni ipi hukum ya kuongeza kuoa wake wengi? Je, ni jambo la msingi au ni ruhusa tu? Kama ni ruhusa ni dharurah gani inayoifanya kuwa ruhusa?
Jibu: Kuoa wake wengi ni matendo ya kujikurubisha mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na ni utiifu, na si ruhusa tu. Kuoa wake wengi ni kujikurubisha kwa Allaah na utiifu na pia ni matendo mema. Ndani yake kuna kuufanya ummah kuwa mkubwa, kuwastiri wanaume na wanawake, ndani yake kuna kuondoa sababu za ufisadi na uzinzi. Amesema (´Azza wa Jall):
وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ
“Mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu kwa mayatima, basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine; wawili au watatu au wanne.”[1]
Yeye (´Azza wa Jall) ameamrisha kuoa wawili, watatu na wanne. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alioa wanawake tisa ambapo akafariki akiwa juu ya wanawake tisa na pia alioa wanawake wawili waliotangulia na alikuwa na wajakazi wawili. Makusudio ni kwamba kuoa wake wengi ni jambo linalotakiwa pamoja na uwezo juu yak na pamoja na uadilifu katika jambo hilo. Akiwa na uwezo na ni mwenye uadilifu, basi imesuniwa kwake kuoa wake wengi ili ummah uwe mkubwa na ili awe na kinga zaidi kwa tupu yake, kinga zaidi kwa macho yake, awastiri wanawake ambao Allaah amemfanyia wepesi kuwastiri na ili kuongezeke kwa sababu hiyo kizazi na ummah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Oeni wanawake wenye mapenzi na wanaozaa sana, kwani hakika mimi nitajifaharisha nanyi juu ya nyumati siku ya Qiyaamah.”
Imekuja katika tamko jengine:
”Nitawazidisha nanyi Manabii siku ya Qiyaamah.”
Kuoa wake wengi kwa wanaomwabudu Allaah duniani, wanaotengeneza duniani na wanaotekeleza nafasi za Mitume katika yale waliyolingania, hili ni kheri kubwa. Tunamuomba Allaah awawafikishe waislamu katika uongofu, usawa na wake wema na waume wema. Inapopatikana mume mwema na mke mwema, basi hiyo ni kheri nyingi na manufaa makubwa. Ni jambo linalotambulika vyema ya kwamba watu wanaweza kujaribiwa kwa vita, maradhi na mambo mengineyo. Kwa hiyo kuoa wake wengi kuna manufaa mengi: mume Allaah humkinga kwayo tupu na macho yake. Kwani mwanamke hujaribiwa kwa maradhi, hujaribiwa kwa hedhi na damu ya uzazi, hujaribiwa kwa mambo yanayomzuia mume kustarehe naye. Kwa hiyo ikiwa ana mke wa pili, wa tatu na wa nne, basi huburudika na wote na kutimiza haja yake, katika kustiri tupu yake na katika kuinamisha chini macho yake. Vivyo hivyo wanawake wanaweza kujaribiwa kwa umaskini na wanaweza kujaribiwa kwa vita. Ikiwa wako chini ya mume anayewasimamia, kuwafanyia wema, kuwaepusha na machafu na kuwalinda, robo ya mume, theluthi ya mume au nusu ya mume ni bora kwao kuliko kutopata kabisa.
Manufaa katika hili ni mengi pamoja na uadilifu, kusimama sawasawa, kumcha Allaah na kutoa nasaha. Ndani ya hili kuna kheri nyingi. Lakini pamoja na dhuluma na uonevu haijuzu kwake. Bali inajuzu na imesuniwa pamoja na uadilifu, kusimama sawasawa na kufanya uadilifu wa mume kwao na uadilifu baina yao katika matumizi juu yao na katika mambo yao yote.
[1] 04:03
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1186/هل-تعدد-الزوجات-اصل-ام-رخصة
- Imechapishwa: 20/04/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1186/هل-تعدد-الزوجات-اصل-ام-رخصة
Imechapishwa: 20/04/2026
https://firqatunnajia.com/kuoa-wake-wengi-ni-jambo-la-msingi-au-ruhusa-tu/