Swali: Ni ipi hukumu ya kuchukua pesa kwa ajili ya kufanya matendo mema?
Jibu: Kuchukua pesa kwa ajili ya kufanya matendo mema kumegawanyika sampuli tatu:
1 – Hayo yafanyike kupitia mkataba kwa maana kwamba yule mtendaji akakubaliana na yule mtoa pesa juu ya fungamano la mshahara kwa mkabala wa matendo mema. Maoni sahihi ni kwamba aina hiyo haisihi. Ni kama mfano wa mtu kupokea mshahara kwa ajili ya kutoa adhaana au kuswalisha, hilo ni kwa sababu kitendo kinachofanywa kwa ajili ya Aakhirah haijuzu kikawa ni njia ya kuitafuta dunia. Allaah (Ta´ala) amesema:
بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ
”Bali mnayapa kipaumbele maisha ya dunia, ilihali Aakhirah ni bora zaidi na ya kudumu zaidi.”[1]
2 – Ambaye anafanya kitendo chema akapokea pesa kwa njia ya tuzo. Mfano wa hilo ni kama mtu kuuliza kama kuna mtu ambaye anataka kutoa adhaana au kuswalisha na atapokea pesa. Maoni sahihi ni kwamba kitendo hicho kinafaa kwa sababu kitendo hicho sio ukodishaji wala sio kufanya fungamano.
3 – Malipo yakawa yanatoka kwenye mamlaka. Kitendo hicho kinafaa na wala hapana shaka. Kwa sababu mosi ni kwamba ni miongoni mwa gharama kwa mujibu wa Shari´ah kutoka katika wizara ya fedha, pili mtendaji anastahiki malipo hayo kutokana na kazi hiyo. Kwa hivyo hapana vibaya akiyacpokea. Pamoja na hivyo inapaswa itambulike kuwa kitendo chake kisifanywe kwa lengo la kutaka pesa; ikiwa kimefanywa kwa lengo la kutaka pesa, basi mshahara huo utakuwa ni haramu. Licha ya hivo haimdhuru kitu endapo atapokea malipo ili yamsaidie kumtii Allaah na kufanya kitendo chake.
[1] 87:16-17
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/164-165)
- Imechapishwa: 20/04/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/164-165)
Imechapishwa: 20/04/2026
https://firqatunnajia.com/matendo-mema-kwa-mkabala-wa-malipo/