Kunyoa ndevu kwa anayekhofia juu ya nafsi yake

Swali: Ambaye anachelea juu ya nafsi yake na kuona kwamba asiponyoa ndevu zake atafungwa?

Jibu: Hapana. Hayo ni katika shaytwaan na shaytwaan kumtia khofu. Lakini akitenzwa nguvu jambo lake linajulikana hata kama inahusiana na shirki:

مَن كَفَرَ بِاللَّـهِ مِن بَعْدِ إِيمَانِهِ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ

“Atakayemkufuru Allaah baada ya kuamini kwake – isipokuwa yule aliyetenzwa nguvu na huku moyo wake umetua juu ya imani.”[1]

Kulazimishwa ambako mtu anapigwa kuna hukumu yake.

Muulizaji: Yeye anaogopa tu?

Ibn Baaz: Hapana, sio udhuru. Unafikri kuwa kutenzwa nguvu inakuwa namna hii tu?

Muulizaji: Kutenzwa nguvu inakuwa kwa kitendo?

Jibu: Inakuwa kwa kupigwa, kufungwa jela na kutishiwa kutoka kwa mtu aliye na uwezo.

[1] 16:106

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23891/حكم-حلق-اللحية-لمن-خاف-على-نفسه
  • Imechapishwa: 25/05/2024