Swali: Kundi la wafanyakazi wanasikia adhaana kisha wanaswali mkusanyiko ndani ya kampuni. Je, kitendo chao hiki ni sahihi?

Jibu: Ni wajibu juu ya wanaume wote kuswali pamoja na mkusanyiko msikitini. Haijuzu kwao kuswali majumbani mwao wala mahali pa kazi ikiwa msikiti uko karibu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote mwenye kusikia mwito kisha asiutikie, basi hana swalah isipokuwa kwa udhuru.” Akaulizwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa): ”Udhuru ni nini?” Akasema: “Khofu au maradhi.”

Bwana mmoja kipofu alimjia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Mimi sina wa kuniongoza kwenda msikitini. Je ninayo ruhusa niswali nyumbani kwangu?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Je unasikia mwito wa swalah?” Akasema: ”Ndio.” Akasema: “Basi itikia.”

Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/120)
  • Imechapishwa: 02/03/2026