Kunakusudiwa kuziswali mara moja au kudumu kuziswali?

Swali 241: Je, ni sharti kudumu kuswali Rak´ah kumi na mbili kila mchana na usiku (Hadiyth aliyopokea Umm Habiybah[1]) au inatosha kuziswali mara moja ili kupata fadhilah hiyo?

Jibu: Kuna mitazamo miwili inayopishana ya wanazuoni kuhusu hilo.

[1] Umm Habiybah Ramlah bint Abiy Sufyaan (Radhiya Allaahu ´anhumaaa) amesimulia kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Hakuna mja yeyote muislamu anayeswali kila siku kwa ajili ya Allaah Rak´ah kumi na mbili ambazo ni za kujitolea – na sio zile za faradhi – isipokuwa Allaah (Ta´ala) atamjengea nyumba Peponi au atajengea nyumba Peponi.”

Ameipokea Muslim, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy na at-Tirmidhiy ambaye amezidisha:

“Rak´ah nne kabla ya Dhuhr, mbili baada yake, mbili baada ya Maghrib, mbili baada ya ´Ishaa na mbili kabla ya swalah ya Fajr.” (Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (579).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 95
  • Imechapishwa: 08/05/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´