Swali: Watu walioathirika na fikira za al-Ikhwaan al-Muslimuun daima wanajengea hoja kwa mfumo wa kukusanya/kulegeza (التمييع) kwa njia ya tofauti na kwamba wanazuoni wametofautiana ili zisikaripiwe zile Bid´ah na makosa walionayo. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Kuna tofauti kati ya tofauti za wanazuoni za hapo kale na tofauti za sasa. Wanazuoni walikuwa wanaweza kutofautiana juu ya swalah inatakiwa kuanza kwa kutaja jina la Allaah kwa sauti ya juu au kuisema kimyakimya, kama nyama ambayo haikutajiwa jina la Allaah inaliwa au hailiwi, kama wudhuu´ ambao mtu hakuanza kutaja jina Allaah unasihi au hausihi, kama Suurah “al-Faatihah” inasomwa nyuma ya imamu anayesoma kwa sauti ya juu au haisomwi na kadhalika. Kuna tofauti kati ya makinzano ya wanazuoni wa kale na tofauti za leo. al-Ikhwaan al-Muslimuun wana kasoro katika ´Aqiydah. Hapa Yemen wanapambana kwa ajili ya kuingia ndani ya bunge ambalo linazingatiwa kuwa ni la Twaaghuut. Wanatambua kufaa kwa mfumo wa makundi mengi – jambo ambalo pia ni Twaaghuut. Mmoja wa viongozi wao, Muhammad bin ´Ajlaan, alisema kuwa atajadili juu ya zulia la demokrasia. Demokrasia ni kufuru, kwa sababu maana yake ni kwamba mtu anahukumu kwa sheria zilizotungwa na watu. Wameingia ndani ya makubaliano ambapo hakuna chama kinachoruhusu kukizungumza vibaya kingine.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 405-406
  • Imechapishwa: 25/06/2025