Kuna mambo ya kijinga kwenye vitabu vya Rabiy´ al-Madkhaliy? – Ibn Baaz anajibu

“Kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz kwenda kwa muheshimiwa ndugu, Dr. Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy – Allaah Amuwafikishe kwa yale yanayomridhisha na Amzidishie elimu na imani yake. Aamiyn!

Salaamun ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh.

Amma ba´d:

Ninakufikishia jibu la muheshimiwa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy kuhusu kitabu chenu “Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Naqd-ir-Rijaal wal-Kutub wat-Twawaaif”, kwa kuwa nilimwacha yeye afanye hilo kutokana na kutokuweza kwangu mimi kufanya hivo. Amejibu kwa mujibu wa aliyoyaona humo. Jibu lake limenifurahisha na himdi zote njema ni za Allaah. Ninamuomba Allaah Atujaalie sisi, nyinyi na ndugu zetu wengine kuwa katika walinganizi wa uongofu na wenye kuinusuru haki.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdilaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Naqd-ir-Rijaal wal-Kutub wat-Tawaa’if, uk. 7
  • Imechapishwa: 05/07/2020