Katika Qur-aan Allaah amemkaripia yule mwenye kumuomba mwingine asiyeweza kumuitikia du´aa yake. Allaah (Ta´ala) amesema:
ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۚ وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ
“Huyo ndiye Allaah, Mola wenu, ufalme ni wake pekee; na wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki hata kijiwavu cha kokwa ya tende. Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu na hata kama watasikia, hawakuitikieni na siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu na wala hakuna awezaye kukupasha khabari vilivyo kama Yule mwenye wa khabari zote.”[1]
Allaah anasema hivi pamoja na kwamba masanamu yapo. Wakati mwingine kulikuwa kunakuwa na mashaytwaan ndani yao wanaojionyesha na kuzungumza na watu. Mwenye kuzungumza na mtu asiyekuwepo ni mbaya zaidi kuliko yule mwenye kuzungumza na kitu kilichopo na kisichokuwa na uhai. Mwenye kumuomba al-Mahdiy ambaye hakuumbwa na Allaah ni mpotevu zaidi kuliko yule mwenye kuyaomba masanamu haya.
Ikiwa watasema kuwa wao wanaamini juu ya kuwepo kwa al-Mahdiy, basi watakuwa katika manzilah moja na wale wenye kuonelea kwamba masanamu yao yatawaombea mbele ya Allaah. Wanaabudu badala ya Allaah visivyoweza kuwanufaisha wala kuwadhuru na huku wanasema: “Watu hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah”.
[1] 35:13-14
- Mhusika: Shaykh-ul-Islam Ahmad bin Taymiyyah
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (1/46-47)
- Imechapishwa: 11/12/2018
Katika Qur-aan Allaah amemkaripia yule mwenye kumuomba mwingine asiyeweza kumuitikia du´aa yake. Allaah (Ta´ala) amesema:
ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۚ وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ
“Huyo ndiye Allaah, Mola wenu, ufalme ni wake pekee; na wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki hata kijiwavu cha kokwa ya tende. Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu na hata kama watasikia, hawakuitikieni na siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu na wala hakuna awezaye kukupasha khabari vilivyo kama Yule mwenye wa khabari zote.”[1]
Allaah anasema hivi pamoja na kwamba masanamu yapo. Wakati mwingine kulikuwa kunakuwa na mashaytwaan ndani yao wanaojionyesha na kuzungumza na watu. Mwenye kuzungumza na mtu asiyekuwepo ni mbaya zaidi kuliko yule mwenye kuzungumza na kitu kilichopo na kisichokuwa na uhai. Mwenye kumuomba al-Mahdiy ambaye hakuumbwa na Allaah ni mpotevu zaidi kuliko yule mwenye kuyaomba masanamu haya.
Ikiwa watasema kuwa wao wanaamini juu ya kuwepo kwa al-Mahdiy, basi watakuwa katika manzilah moja na wale wenye kuonelea kwamba masanamu yao yatawaombea mbele ya Allaah. Wanaabudu badala ya Allaah visivyoweza kuwanufaisha wala kuwadhuru na huku wanasema: “Watu hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah”.
[1] 35:13-14
Mhusika: Shaykh-ul-Islam Ahmad bin Taymiyyah
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (1/46-47)
Imechapishwa: 11/12/2018
https://firqatunnajia.com/kumwamini-al-mahdiy-anayesubiriwa-ni-kama-kuyaamini-masanamu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)