Swali: Ikiwa mtu anakula na mtu mwenye ugonjwa wa ngozi (ukoma) au anakaa naye hali ya kuwa ni mwenye kumtegemeya Allah, je, anapata dhambi?

Jibu:  Hakuna ubaya, ikiwa ni kwa faida, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomjia bwana mmoja mwenye ukoma:

“Kwa jina la Allaah, hali ya kumtegemea Allaah.”

na akala nae. Kufanya sababu ni jambo linalotakikana. Na ikiwa mtu atahitaji kuwa pamoja na mgonjwa huyo, kwa lengo la kumuhudumia au kwa ajili ya kumpa matibabu, hakuna ubaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/22027/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D8%AE%D8%A7%D9%84%D8%B7%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%AC%D8%B0%D9%88%D9%85-%D9%88%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D9%8A%D8%B6-%D9%84%D8%AD%D8%A7%D8%AC%D8%A9
  • Imechapishwa: 08/06/2020