an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema katika “al-Majmuu´” (05/144, 258):
“Kumswalia kafiri na kumuombea du´aa ya msamaha ni haramu kwa andiko la Qur-aan na kwa maafikiano.”
Kutokana na hayo utatambua makosa ya baadhi ya waislamu hii leo ambapo wanawaombea du´aa ya rehema na kuwaombea radhi baadhi ya makafiri. Hayo yanafanyika kwa wingi kutoka kwa baadhi ya watu wa magazeti na majarida. Hakika mimi nimemsikia mmoja katika waarabu wanaojulikana akimuombea rehema Staaliyn, ambaye ni mkomunisti ambaye yeye na madhehebu yake, ni katika maadui wakubwa zaidi dhidi ya dini. Hayo aliyafanya katika kalima ya raisi ambaye punde ameashiriwa katika mnasaba wa kufa kwa mtu aliyetajwa ambayo ilirushwa redioni. Hakuna mshangao kutokana na mtu kwa sababu pengine hukumu kama hii inaweza kuwa si yenye kutambulika kwake. Kilicho mshangao ni kwa baadhi ya walinganizi wa Kiislamu kutumbukia katika jambo kama hilo ambapo amesema katika kijitabu chake:
“Allaah amrehemu Bernard…. “
Nimepewa khabari na baadhi ya watu ninaowaamini kwamba mmoja katika Mashaykh alikuwa akimswalia mmoja katika wanaokufa katika pote la Ismaa´iyliyyah Baatwiniyyah pamoja na kwamba yeye anaonelea kuwa sio waislamu. Kwa sababu watu hao hawaonelei kuwepo kwa swalah, hajj na wanamwabudu mtu. Pamoja na hayo anawaswalia kwa njia ya unafiki na kujikombakomba kwao. Allaah ndiye mwenye kushtakiwa na ndiye mwenye kutakwa msaada.”
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 123-124
- Imechapishwa: 12/04/2020
an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema katika “al-Majmuu´” (05/144, 258):
“Kumswalia kafiri na kumuombea du´aa ya msamaha ni haramu kwa andiko la Qur-aan na kwa maafikiano.”
Kutokana na hayo utatambua makosa ya baadhi ya waislamu hii leo ambapo wanawaombea du´aa ya rehema na kuwaombea radhi baadhi ya makafiri. Hayo yanafanyika kwa wingi kutoka kwa baadhi ya watu wa magazeti na majarida. Hakika mimi nimemsikia mmoja katika waarabu wanaojulikana akimuombea rehema Staaliyn, ambaye ni mkomunisti ambaye yeye na madhehebu yake, ni katika maadui wakubwa zaidi dhidi ya dini. Hayo aliyafanya katika kalima ya raisi ambaye punde ameashiriwa katika mnasaba wa kufa kwa mtu aliyetajwa ambayo ilirushwa redioni. Hakuna mshangao kutokana na mtu kwa sababu pengine hukumu kama hii inaweza kuwa si yenye kutambulika kwake. Kilicho mshangao ni kwa baadhi ya walinganizi wa Kiislamu kutumbukia katika jambo kama hilo ambapo amesema katika kijitabu chake:
“Allaah amrehemu Bernard…. “
Nimepewa khabari na baadhi ya watu ninaowaamini kwamba mmoja katika Mashaykh alikuwa akimswalia mmoja katika wanaokufa katika pote la Ismaa´iyliyyah Baatwiniyyah pamoja na kwamba yeye anaonelea kuwa sio waislamu. Kwa sababu watu hao hawaonelei kuwepo kwa swalah, hajj na wanamwabudu mtu. Pamoja na hayo anawaswalia kwa njia ya unafiki na kujikombakomba kwao. Allaah ndiye mwenye kushtakiwa na ndiye mwenye kutakwa msaada.”
Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 123-124
Imechapishwa: 12/04/2020
https://firqatunnajia.com/kumuombea-kafiri-msamaha-na-rehema-baada-ya-kufa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)