Swali: Ni shirki mtu akimuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hayuko mbele ya kaburi lake? Je, hukumu inatofautiana mtu akimuomba ilihali yuko mbele ya kaburi lake?
Jibu: Hapana, hukumu haitofautiani. Kumuomba asiyekuwa Allaah, popote pale, ni shirki. Haijalishi kitu mtu akiwa makaburini au mahala kwengine. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا
“Kwamba mahala kote pa kuswalia ni kwa ajili ya Allaah pekee, hivyo basi msiombe yeyote pamoja na Allaah.” (72:18)
فَادْعُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ
“Basi mwombeni Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini.” (40:14)
Ni lazima kumtakasia ´ibaadah katika du´aa pahali kokote. Hili halihusiani na kwenye makaburi peke yake.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2105
- Imechapishwa: 30/06/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)