Kumuomba Allaah akuingize Peponi bila hesabu wala adhabu

Swali: Ni ipi hukumu ya kuomba kwa wingi:

“Ee Allaah! Niingize Peponi bila hesabu wala adhabu?”

Kwa vile haikupokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Jibu: Huku ni kuchupa mipaka katika kuomba du´aa. Kwa sababu inatambulika kwamba wale watakaoingia Peponi bila hesabu wala adhabu wamehakikisha sharti maalum. Kilichopokelewa ni:

اللهم إني أسألك الجنة

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba Pepo.”[1]

[1] as-Swahiyhah (1542) na Swahiyh Sunan Ibn Maajah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 279
  • Imechapishwa: 04/07/2022