Swali: Je, inafaa kumuoa mwanamke mzinzi ambaye aliadhibiwa?

Jibu: Ikitambulika kuwa ametubu inafaa kwako kumuoa. Lakini ikiwa hujui kuwa alitubu, basi tambua kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) anasema:

الزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ ۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ

“Mwanamme mzinifu hafungi ndoa isipokuwa na mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina na mwanamke mzinifu haolewi isipokuwa na mwanamme mzinifu au mshirikina – na yameharamishwa hayo kwa waumini.”[1]

[1] 24:03

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 251
  • Imechapishwa: 10/03/2025