Swali 30: Kuna mtu ni muislamu ambaye amemuoa mkriso kisha wakafunga ndoa kanisani. Ni ipi hukumu yake?

Jibu: Wafunge ndoa upya kwa waislamu. Baba yake mwanamke akiwa ni kafiri basi hana usimamizi juu yake. Ateue mmoja katika waislamu na wafunge ndoa upya kwake. Endapo watafunga ndoa mbali na kanisani basi ndio bora zaidi[1]. Bali kilicho cha wajibu waislamu wajitosheleza na maadui wa Uislamu na watakwe jambo hilo.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/kufunga-ndoa-na-mwanamke-wa-kinaswara-kanisani/

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 70-71
  • Imechapishwa: 22/12/2019