Kumtaja Allaah sehemu ya kutawadhia

Swali: Je, inajuzu kumtaja Allaah ndani ya choo?

Jibu: Haitakikani kwa mtu kumtaja Mola wake ndan ya choo. Kwa sababu ana uwezo wa kufanya kinyume na hivo. Akimtaja kwa moyo wake ni sawa pasi na kumtaja kwa moyo wake. Vinginevyo bora zaidi asitamke kwa mdomo wake sehemu hii. Asubiri mpaka atapotoka nje.

Lakini ni sawa kumtaja Allaah ikiwa ni sehemu ya kutawadhia peke yake ambako kumetengana na sehemu ya kukidhia haja.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (07) http://binothaimeen.net/content/6706
  • Imechapishwa: 26/11/2020