Swali: Suufiyyah humtaja Allaah kwa dhamiri pekee wakisema “Yeye, Yeye”?

Jibu: Hii ni Bid´ah, si miongoni mwa nyiradi. Kama kusema “Allaah, Allaah” bila muundo kamili wa Dhikr, hiyo si Dhikr. Dhikr sahihi ni kama “Subhaan Allaah”, “Laa ilaaha illa Allaah”, kama ilivyokuja katika maandiko. Kwa sababu ´ibaadah inakuwa kwa mujibu wa dalili. Haziwezi kufanywa kwa kubuni. Lakini njia za kufikia Dhikr kwa kufikiria na kuzingatia ni jambo limewekwa katika Shari´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31187/ما-حكم-ذكر-الله-بالضمير-المجرد-هو-هو
  • Imechapishwa: 10/10/2025