Kumtahiri mtoto kabla ya siku saba tangu kuzaliwa kwake

Swali 8378: Je, inajuzu kumtahiri mtoto kabla ya kutimiza siku saba tangu kuzaliwa kwake, khaswa kwa kuwa katika baadhi ya hospitali hufanya tohara kabla ya kutimiza siku saba? Mtu mmoja aliniambia kwamba ni haramu kumtahiri kabla ya siku saba na kwamba inachukiza baada ya siku saba. Je, hilo ni kweli?

Jibu: Kumtahiri mtoto ni Sunnah. Si haramu kumtahiri kabla ya siku ya saba wala hakuna machukizo. Wala si haramu kuichelewesha baada ya siku hiyo wala haichukizwi. Jambo hilo ni lenye wasaa, huku ikizingatiwa maslahi ya mtoto. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mambo matano ni katika maumbile: tohara, kunyoa nywele za sehemu za siri, kupunguza masharubu, kukata kucha na kung’oa nywele za kwapani.”[1]

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.

[1] Ahmad (02/229), al-Bukhaariy (07/56) na Muslim (01/153) na wengineo.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/111)
  • Imechapishwa: 21/10/2026