Swali: Je, anaswaliwa aliyejiua, mwenye kuacha kuswali msikitini na mla ribaa? Je, anaswaliwa aliyeuawa kwa kutekelezewa adhabu ya kidini?
Jibu: Kanuni ni kwamba mwenye kufanya maasi ambaye si kafiri anaswaliwa. Lakini ikiwa watu wakubwa kama mwanazuoni, hakimu au kiongozi wataacha kumswalia kwa ajili ya kuwaonya wengine na kuwafanya wachukie kitendo hicho kibaya, kama kula ribaa au kujiua, basi hilo ni kwa ajili ya kuonya. Vinginevyo kimsingi anaswaliwa. Lakini aliyeuawa kwa adhabu ya kidini kama mfano wa adhabu ya uzinzi kwa aliyeoa, hawa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalia, kwa sababu huyu ametubia na adhabu ni tawbah yenye kufuta madhambi.
Mwenye kuacha swalah ni kafiri na hivyo haswaliwi. Asiyeswali haswaliwi kwa sababu ni kafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ahadi iliyoko baina yetu na wao ni swalah. Hivyo basi yeyote atakayeiacha basi amekufuru.”
Ikiwa anajulikana kuwa haswali kabisa, hajali swalah wala kuipa umuhimu au anakataa kuwa ni wajibu, basi huyu ni kafiri. Tunamuomba Allaah atupe usalama. Kuhusu anayeswali nyumbani lakini haswali mkusanyiko msikitini, huyu ni mtenda dhambi na hivyo anaswaliwa.
Swali: Nitajuaje kama anaswali nyumbani au haswali?
Jibu: Hili linahitaji kutazamwa. Ikiwa mtu anaonekana kuwa mtu mwema, yuko pamoja na waislamu, ingawa humuoni msikitini, huenda anaswali msikiti mwingine au watu wanamshuhudia kwa kheri. Kusudio ni kuwa jambo hili linahitaji uangalifu. Asiyejulikana misikitini anaweza kudhaniwa vibaya – tunamwomba Allaah salama – lakini hakuhukumiwi kuwa kafiri moja kwa moja. Hakuna ubaya kumswalia muda wa kuwa yuko pamoja na waislamu na anashuhudia kuwa hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Anachukuliwa kama muislamu mpaka ijulikane wazi kuwa haswali kabisa.
Swali: Aliyeuawa kwa adhabu ya kidini au kwa kisasi anaswaliwa na kuzikwa kaburini?
Jibu: Ndiyo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1013/حكم-الصلاة-على-مرتكب-الكباىر
- Imechapishwa: 09/01/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1013/حكم-الصلاة-على-مرتكب-الكباىر
Imechapishwa: 09/01/2026
https://firqatunnajia.com/kumswalia-mtenda-dhambi-kubwa/