Kumposa mwanamke aliyeachika mara tatu ndani ya eda

Swali: Ikiwa mwanamke ameshaachika talaka tatu mtu amwekee wazi juu ya kumposa ndani ya eda au amwashirie?

Jibu: Ikiwa ameshaachika talaka tatu… bora zaidi ni kumwashiria. Kwa sababu sio wakati wa ndoa. Bado yuko ndani ya eda. Udhahiri wa dalili ni kuenea. Kwani bado yuko ndani ya wakati ambao ndoa ni haramu.

Swali: Je, mtu anaweza kusema kuwa inafaa au inapendeza kumtazama mposwaji?

Jibu: Inapendeza. Inapendeza kumtazama yule mwanamke mposwaji. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamrisha jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23826/حكم-خطبة-المطلقة-طلاقا-باىنا-في-العدة
  • Imechapishwa: 07/05/2024