Swali: Mtu akimpenda mke wake kwa ajili ya dini na tabia yake anapewa thawabu kwa mapenzi haya? Vipi ikiwa atampenda kwa sababu ya urembo wake anapata dhambi kwa hilo?

Jibu: Hapana, hapati dhambi kwa hilo. Lakini hata hivyo ikiwa anampenda kwa sababu ni mwenye kumtii Allaah na Mtume wake ndio mapenzi yaliyo juu zaidi. Kwa sababu ni mapenzi ya kidini. Kuhusu yale ya kwanza ni mapenzi ya kimaumbile. Kumpenda kwa sababu ya urembo wake ni mapenzi ya kimaumbile. Akimpenda kwa sababu ni mchaji Allaah na kwa sababu ni muumini ni mapenzi ya kidini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (72) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighassat%20-11-01-1439h.mp3
  • Imechapishwa: 16/12/2017