Kumpa nasaha ndugu yako muislamu ni lazima ikiwa hajakushauri?

Swali: Je, nasaha za wajibu zinazingatiwa ni pale mtu anapokuomba au ni mtu mwenyewe kujitolea nazo bila ya kuombwa?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Dini ni kupeana nasaha. Dini ni kupeana nasaha. Dini ni kupeana nasaha.”[1]

Kwa hivyo ikiwa unajua kwamba ndugu yako amefanya jambo na anahitaji ushauri, inapaswa kumshauri. Na ikiwa atakuomba ushauri, basi mshauri. Ni kitu kimekokotezwa. Kwa maana nyingine ni kwamba akikutaka ushauri jambo fulani, basi haifai kumdanganya. Vinginevyo ikiwa yeye hajakuuliza, inapaswa kumshauri bila yeye kuomba. Hii ni Sunnah iliyosisitizwa. Unapaswa kumshauri ikiwa unamwona akielekea kufanya jambo linaloweza kumdhuru, anapojihusisha na bidhaa isiyofaa au inayodanganya. Kitu chochote ambacho unaona kina manufaa na ndugu yako unapaswa kumshauri kuhusu kitu hicho, na nasaha zinaweza kuwa za lazima, inategemea hali.

[1] Muslim (55).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25261/هل-النصيحة-مقيدة-بطلبها-ام-تبذل-دون-طلب
  • Imechapishwa: 23/02/2025