Swali: Baadhi ya wagonjwa wanawaambia wenye kufanya matabano kwamba hawatowapa malipo isipokuwa baada ya kuponywa na Allaah. Je, sharti hii inafaa?

Jibu: Ndio, inafaa kwa mgonjwa kumuwekea sharti anayefanya matabano kumpa kitu fulani baada ya kuponywa na Allaah. Vinginevyo hatompa kitu.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/40)
  • Imechapishwa: 15/05/2026