Swali: Ikiwa ninafanya kazi fulani na nalipwa kwa kazi hiyo, lakini ikatokea nikawa na kazi nyingine ambapo nikamuomba mtu mwingine aifanye kazi yangu hiyo na achukue nusu ya mshahara wangu nami nichukue nusu iliyobaki. Je, hili linajuzu?
Jibu: Ikiwa kinachokusudiwa katika mkataba ni kupatikana kwa kazi yenyewe, yaani kazi ifanyike na lengo litimie na wewe ukamwajiri mtu wa kuifanya kwa namna ileile unavyoweza kuifanya wewe, aliye sawa na wewe au bora zaidi yako, basi hakuna tatizo. Isipokuwa kama yule aliyekuajiri alitaka wewe binafsi ndiye uifanye kazi hiyo na akashurutisha wazi kwamba lazima uifanye mwenyewe au alitaka kazi ifanywe kwa mkono wako binafsi. Katika hali hii, haijuzu kumuajiri mtu mwingine badala yako. Ama ikiwa sivyo, yaani hakukusudiwa wewe binafsi, bali kilichokusudiwa ni kupatikana kwa kazi yenyewe – kama kujenga chumba, kurekebisha mlango, kufungua tundu au mfano wa hayo – na alipokubaliana nawe alikusudia kazi itekelezwe, hata kama si kwa mikono yako mwenyewe, bali kwa mfanyakazi mwingine, basi katika hali hiyo ukimuajiri mfanyakazi atekeleze jukumu hilo kama wewe au bora zaidi yako, basi hapana vibaya. Hata iwe umemlipa kwa kiasi kilekile unacholipwa, kwa kidogo au kwa zaidi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2145/حكم-من-اقام-غيره-على-عمل-واعطاه-نصف-الراتب
- Imechapishwa: 02/01/2026
Swali: Ikiwa ninafanya kazi fulani na nalipwa kwa kazi hiyo, lakini ikatokea nikawa na kazi nyingine ambapo nikamuomba mtu mwingine aifanye kazi yangu hiyo na achukue nusu ya mshahara wangu nami nichukue nusu iliyobaki. Je, hili linajuzu?
Jibu: Ikiwa kinachokusudiwa katika mkataba ni kupatikana kwa kazi yenyewe, yaani kazi ifanyike na lengo litimie na wewe ukamwajiri mtu wa kuifanya kwa namna ileile unavyoweza kuifanya wewe, aliye sawa na wewe au bora zaidi yako, basi hakuna tatizo. Isipokuwa kama yule aliyekuajiri alitaka wewe binafsi ndiye uifanye kazi hiyo na akashurutisha wazi kwamba lazima uifanye mwenyewe au alitaka kazi ifanywe kwa mkono wako binafsi. Katika hali hii, haijuzu kumuajiri mtu mwingine badala yako. Ama ikiwa sivyo, yaani hakukusudiwa wewe binafsi, bali kilichokusudiwa ni kupatikana kwa kazi yenyewe – kama kujenga chumba, kurekebisha mlango, kufungua tundu au mfano wa hayo – na alipokubaliana nawe alikusudia kazi itekelezwe, hata kama si kwa mikono yako mwenyewe, bali kwa mfanyakazi mwingine, basi katika hali hiyo ukimuajiri mfanyakazi atekeleze jukumu hilo kama wewe au bora zaidi yako, basi hapana vibaya. Hata iwe umemlipa kwa kiasi kilekile unacholipwa, kwa kidogo au kwa zaidi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2145/حكم-من-اقام-غيره-على-عمل-واعطاه-نصف-الراتب
Imechapishwa: 02/01/2026
https://firqatunnajia.com/kumpa-kazi-yako-mtu-mwengine-na-ukampa-nusu-ya-mshahara-wako/