Hataki kumnasihi mtenda maasi kwa sababu anajua hukumu

Swali: Ni ipi hukumu nikimuona mtu anafanya dhambi nisimnasihi kwa hoja eti anajua hukumu yake?

Jibu: Mtu anafanya dhambi na anajua, lakini hilo ni kutokana na ujinga wa mtu. Ujinga ndio unaotawala moyo wake wakati wa kufanya dhambi hiyo na hivyo akasahau adhabu na matishio ya Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّمَا التَّوْبَةُ عَلَى اللَّـهِ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السُّوءَ بِجَهَالَةٍ

“Hakika si vengienvyo tawbah inayopokelewa na Allaah ni ya wale ambao wanafanya uovu kwa ujahili.” (04:17)

Amewasifu ujinga ijapo watakuwa ni wenye kujua yale wanayoyafanya. Lakini mtu anatiwa ujinga moyoni mwake kile kipindi cha kuyafanya maasi na hivyo akasahau utukutu wa Allaah, ukamilifu wa ujuzi wa Allaah, utambuzi wa Allaah juu yake na kwamba Allaah anamuona na anajua ya siri na ya dhahiri yake. Kwa hivyo hali hizo zinampotea. Ni lazima kumnasihi na kumtahadharisha ghadhabu za Allaah ili kutekeleza lile jukumu lililo juu yako ambalo ni kulingania kwa Allaah:

“Yeyote katika nyinyi mwenye kuona maovu, basi ayazuie kwa mkono wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa mdomo wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa moyo wake – na hiyo ni imani dhaifu mno.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/نصيحة-العاصي-الذي-يعلم-الحكم
  • Imechapishwa: 18/06/2022