Swali: Yule anayesema kwamba kumhama mtu ni kama dawa. Kama kunaleta manufaa, basi ndiko kutumike na kama…

Jibu: Ndio, ikiwa kunaleta manufaa, hutumika. Kama vile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyowahama wale watu watatu na Allaah akawanufaisha kwa hilo. Lakini hakumhama ‘Abdullaah bin Ubayy na wenzake, kwa sababu kuhama hakukuwa na manufaa kwao.

Swali: Vipi mtu wa Bid´ah ikiwa mawaidha na uongofu havina athari kwake?

Jibu: Anahamwa.

Swali: Vipi ikiwa kumhama hakumletei manufaa?

Jibu: Ikiwa ipo dola inayosimamisha mambo kwa mujibu wa amri za Allaah, basi jambo lake linafikishwa kwa dola hiyo. Ama wewe binafsi, jukumu lako ni moja kati ya mawili: ama unampa nasaha au unamhama. Lakini huna ruhusa ya kumuua au kumpiga.

Swali: Katika hali hiyo kuhama kumewekwa katika Shari´ah?

Jibu: Ndio, hadi atakapotubia. Hata kama itachukua mwaka mmoja, miwili au hata miaka kumi, mpaka atakapotubia. Ni kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyowakata wale watu watatu kwa muda wa siku khamsini, mpaka Allaah alipokubali tawba yao.

Swali: Maana yake ni kwamba hakuna muda maalum wa kuhama?

Jibu: Ndio, khaswa inapokuja ikiwa ni katika maasi na Bid´ah.

Swali: Je, inategemea manufaa?

Jibu: Inategemea vile atakavyoona mwenye kuhama; akiona kwamba kutohama kutaleta manufaa kwao, basi aendelee kuonana nao na kuwapa nasaha. Lakini akiona kwamba nasaha hazina faida tena, basi anawahama.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31626/ما-ضابط-الهجر-النافع-للعاصي-والمبتدع
  • Imechapishwa: 12/11/2025