Kumfanyia ´Umrah mzazi mzee asiyeweza

Swali: Je, inafa kumfanyia ´Umrah mama yangu ambaye ana zaidi ya miaka sitini na tano na mimi hivi sasa nimekwishatekeleza ile hajj ya kwanza ambayo ni faradhi mwaka huu?

Jibu: Akiwa si muweza wa kuhiji kutokana na utuuzima wake, kutokuwa kwake na uwezo kwa sababu ya maradhi yaliyompata au uzee uliyomkwamisha, basi hakuna neno. Itakuwa haifai kumkalia niaba ikiwa anaweza kutokana na afya yake njema; si katika Hajj wala katika ´Umrah. Kwa sababu ruhusa imepokolewa juu ya yule ambaye ameshindwa kutokana na utuuzima wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4719/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D8%AF%D8%A7%D8%A1-%D8%A7%D9%84%D8%B9%D9%85%D8%B1%D8%A9-%D8%B9%D9%86-%D8%A7%D9%84%D8%B9%D8%A7%D8%AC%D8%B2-%D9%88%D9%83%D8%A8%D9%8A%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D8%B3%D9%86
  • Imechapishwa: 29/11/2020