Swali: Kumchinjia mgeni ni katika kumchinjia asiyekuwa Allaah?

Jibu: Kumkirimu mgeni kunafanywa kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho basi amkirimu mgeni wake.”

Lakini ikiwa mnyama anachinjwa mbele ya mlango ili bibi harusi apite mbele yake ili asipatwe na uchawi wala shaytwaan, basi kichinjwa hicho kimechinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Allaah.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 466
  • Imechapishwa: 01/08/2025