Swali: Nikiwa katika safari ambayo mtu anaweza kufupisha swalah na swalah ya ´Aswr ikanifikia na sikuiswali mpaka wakati wake ulipokwisha na nikafika kwa ahli zangu. Je, nilipe swalah ile kwa kufupisha au kikamilifu?

Jibu: Msafiri akifika kwa ahli zake, analipa swalah zilizompita kikamilifu na hafupishi. Anafupisha tu katika hali yake ya safari, ama akichelewesha kwa mfano ´Aswr, au Dhuhr au ´Ishaa mpaka akafika kwa ahli zake, ataswali Rak´ah nne, kwa kuwa rukhusa alikuwa nayo katika hali ya safari.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 25/03/2018