Swali: Ni ipi hukumu ya usingizi wa alasiri?
Jibu: Hatujui dalili yoyote maalum kuhusu usingizi wa ´Aswr na hakuna tatizo katika hilo. Nyakati zote za kulala hatujui kuwa kuna jambo lililokatazwa, isipokuwa wakati wa Maghrib. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akichukia kulala kabla ya swalah ya ´Ishaa, kwa maana kabla ya swalah ya usiku na pia alikuwa akichukia mazungumzo baada ya swalah ya ´Ishaa. Ama ´Aswr, Dhuhr, Dhuhaa na asubuhi hakuna jambo lolote lililothibiti linalokataza kulala katika nyakati hizo. Lakini mtu ajitahidi kuchagua wakati unaofaa zaidi. Ikiwa ataweza kulala adhuhuri, hilo ni bora kuliko alasiri. Ikiwa ataweza kulala usingizi wa mchana kabla ya Dhuhr hilo ni bora zaidi. Lakini kwa sababu ya kazi za watu wengi siku hizi, wengi hawapati nafasi ya usingizi wa mchana wala ya kulala adhuhuri. Kwa hivyo hubaki na fursa ya kulala baada ya alasiri. Hilo halina tatizo. Ikiwa atalale mwanzoni mwa mchana, hakuna tatizo. Lakini ikiwa ataweza kutolala mara moja baada ya swalah ya asubuhi, bali akae akimtaja Allaah, akisoma Qur-aan au akiwa katika kujifunza elimu mpaka jua lipande, kisha alale kidogo baada ya kuchomoza, basi hilo ni bora zaidi kuliko kulala mara tu baada ya swalah. Hata hivyo hakuna tatizo katika hilo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1641/حكم-النوم-بعد-العصر
- Imechapishwa: 07/06/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya usingizi wa alasiri?
Jibu: Hatujui dalili yoyote maalum kuhusu usingizi wa ´Aswr na hakuna tatizo katika hilo. Nyakati zote za kulala hatujui kuwa kuna jambo lililokatazwa, isipokuwa wakati wa Maghrib. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akichukia kulala kabla ya swalah ya ´Ishaa, kwa maana kabla ya swalah ya usiku na pia alikuwa akichukia mazungumzo baada ya swalah ya ´Ishaa. Ama ´Aswr, Dhuhr, Dhuhaa na asubuhi hakuna jambo lolote lililothibiti linalokataza kulala katika nyakati hizo. Lakini mtu ajitahidi kuchagua wakati unaofaa zaidi. Ikiwa ataweza kulala adhuhuri, hilo ni bora kuliko alasiri. Ikiwa ataweza kulala usingizi wa mchana kabla ya Dhuhr hilo ni bora zaidi. Lakini kwa sababu ya kazi za watu wengi siku hizi, wengi hawapati nafasi ya usingizi wa mchana wala ya kulala adhuhuri. Kwa hivyo hubaki na fursa ya kulala baada ya alasiri. Hilo halina tatizo. Ikiwa atalale mwanzoni mwa mchana, hakuna tatizo. Lakini ikiwa ataweza kutolala mara moja baada ya swalah ya asubuhi, bali akae akimtaja Allaah, akisoma Qur-aan au akiwa katika kujifunza elimu mpaka jua lipande, kisha alale kidogo baada ya kuchomoza, basi hilo ni bora zaidi kuliko kulala mara tu baada ya swalah. Hata hivyo hakuna tatizo katika hilo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1641/حكم-النوم-بعد-العصر
Imechapishwa: 07/06/2026
https://firqatunnajia.com/kulala-baada-ya-alasiri/