Swali: Je, miraa ni katika madawa ya kulevya? Ni ipi hukumu ya kuila?

Jibu: Wanazuoni wengi wametaja kuwa miraa ni katika vitu vinavyolevya na madawa ya kulevya. Imetajwa kuwa asili yake ni Yemen na haijulikani vipi ilivyoenea. Kwa sababu hiyo katika mkutano uliokuwepo hivi karibuni Madiynah al-Munawwarah waliohudhuria walifanya maafikiano juu ya kuharamishwa kwake, kama ilivyo kwa sigara, kutokana na shari na uharibifu unaotokana nayo. Ingawa baadhi ya ndugu zetu wa Yemen walipinga hilo na wakasema madhara yake ni mepesi na haisababishi kulewa. Hata hivyo yule anayeitumia na kuizoea anaweza asitambue shari na uharibifu wake na huenda ikawa vigumu kwake kukiri madhara na uharamu wake. Ama wale ambao Allaah amewaepusha na shari yake na wameifahamu hali yake, wamesema wazi juu ya uharibifu wake na kwamba wakati mwingine hulevya. Pia wametaja kuwa mtumiaji wake anaweza kuchanganyikiwa njia na matokeo yake akapoteza familia yake na watoto wake kutokana na kuitumia. Zaidi ya hayo miraa husababisha kuharibu matendo na shughuli za watu, kwa kuwa wanaokaa muda mrefu wakitafuna, wakihifadhi mdomoni, wakitema na kubaki kwa muda mrefu bila kufanya kazi yoyote kwa sababu ya kujiingiza katika balaa hii.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1636/هل-القات-من-المخدرات-وما-حكم-اكله
  • Imechapishwa: 07/06/2026