Eti kumbusu mwanamke wa kigeni ni dhambi ndogo tu

Swali: Ni ipi jawabu kwa anayesema kwamba kumbusu mwanamke asiye Mahram wako na kufanya naye kila kitu, isipokuwa uzinzi, ni dhambi inayofutwa kwa kuomba msamaha tu?

Jibu: Maneno haya ni uovu na ni jambo lililokataliwa. Kuendelea kulifanya na kulishikilia ni dhambi kubwa. Dhambi kubwa haifutwi kwa kuomba msamaha pekee. Haiifutwi ila kwa tawbah ya kweli. Ikiwa mtu amembusu mwanamke bila haki, naye si Mahram wake, amemgusa au mfano wa hayo, basi hilo halifutwi isipokuwa kwa tawbah. Kuendelea kufanya dhambi kunaigeuza kuwa dhambi kubwa. Ama akitubia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), akaacha kuendelea, akajuta juu ya aliyoyafanya, akahifadhi swalah tano, kuswali ijumaa hadi ijumaa nyingine, kufunga Ramadhaan hadi Ramadhaan nyingine na sambamba na hayo huku akiepuka madhambi makubwa, basi Allaah atamsamehe madhambi madogo ambayo hakuendelea juu yake. Ama akiendelea juu yake, basi hugeuka kuwa madhambi makubwa na hapo ni lazima kuwepo tawbah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1744/لرد-على-من-زعم-ان-تقبيل-المراة-الاجنبية-يمحوه-الاستغفار
  • Imechapishwa: 07/06/2026