Anayekunywa pombe duniani hatoinywa Aakhirah?

Swali: Je, mnywaji wa pombe akitubia kabla ya kufa atainywa katika nyumba ya Aakhirah ikiwa atakuwa miongoni mwa watu wa Peponi?

Jibu: Mtu akitubia basi hukumu ya dhambi huondoka. Kwa hakika anayetubia kutokana na dhambi ni kama asiye na dhambi. Ama yule anayekufa hali ya kuwa bado anakunywa pombe, basi Allaah amempa onyo kali kwamba hatainywa Aakhirah, hata kama ataingia Peponi. Hili ni onyo zito. Lakini yule anayetubia kutokana na pombe, basi Allaah humkubalia tawbah yake. Akitubia kisha akafa juu ya tawbah hiyo, basi Allaah humuepusha na shari yake na hukumu yake huwa kama ya yule ambaye hakuwahi kuinywa kabisa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1637/هل-يحرم-من-خمر-الجنة-من-شربها-في-الدنيا-وتاب
  • Imechapishwa: 07/06/2026