Swali: Je, inajuzu kuunganisha swalah ya Dhuhr na ´Aswr, na Maghrib na ‘Ishaa kwa sababu ya mvua?
Jibu: Inajuzu ikiwa sababu ipo. Mvua inawatia watu mashaka. Hivyo inajuzu kuunganisha Dhuhr na ´Aswr, pamoja na Maghrib na ‘Ishaa. Baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa inajuzu Maghrib na ‘Ishaa tu, kwa sababu Dhuhr na ´Aswr zinaswaliwa mchana na hakuna mashaka sana. Lakini hili si sahihi, kwa kuwa mashaka yanaweza kutokea hata mchana endapo mvua ni kubwa, kuna mafuriko au barabara zimejaa matope. Katika hali kama hizi, inajuzu kwa waislamu kukusanya swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikusanya Dhuhr na ´Aswr, na Maghrib na ‘Ishaa akiwa mjini. Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema alifanya hivyo ili asiitie mashaka ummah wake. Baadhi ya wanazuoni wamesema alikusanya kwa sababu ya utelezi sokoni na wengine wamesema kwa sababu kulikuwa na ugonjwa uliowatatiza watu.
Kwa ujumla ikiwa kuna maradhi, mvua kubwa au jambo linalowasumbua watu, basi aliye na maradhi anaruhusiwa kukusanya baina ya Dhuhr na ´Aswr, pamoja na Maghrib na ‘Ishaa. Vivyo hivyo msafiri, au katika mvua nzito inayowapa watu uzito. Inajuzu kujumuisha kwa kutanguliza au kwa kuchelewesha, ni mamoja iwe wakati wa Dhuhr au ´Aswr, na iwe wakati wa Maghrib au ‘Ishaa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1080/جمع-الصلاتين-في-المطر
- Imechapishwa: 28/01/2026
Swali: Je, inajuzu kuunganisha swalah ya Dhuhr na ´Aswr, na Maghrib na ‘Ishaa kwa sababu ya mvua?
Jibu: Inajuzu ikiwa sababu ipo. Mvua inawatia watu mashaka. Hivyo inajuzu kuunganisha Dhuhr na ´Aswr, pamoja na Maghrib na ‘Ishaa. Baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa inajuzu Maghrib na ‘Ishaa tu, kwa sababu Dhuhr na ´Aswr zinaswaliwa mchana na hakuna mashaka sana. Lakini hili si sahihi, kwa kuwa mashaka yanaweza kutokea hata mchana endapo mvua ni kubwa, kuna mafuriko au barabara zimejaa matope. Katika hali kama hizi, inajuzu kwa waislamu kukusanya swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikusanya Dhuhr na ´Aswr, na Maghrib na ‘Ishaa akiwa mjini. Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema alifanya hivyo ili asiitie mashaka ummah wake. Baadhi ya wanazuoni wamesema alikusanya kwa sababu ya utelezi sokoni na wengine wamesema kwa sababu kulikuwa na ugonjwa uliowatatiza watu.
Kwa ujumla ikiwa kuna maradhi, mvua kubwa au jambo linalowasumbua watu, basi aliye na maradhi anaruhusiwa kukusanya baina ya Dhuhr na ´Aswr, pamoja na Maghrib na ‘Ishaa. Vivyo hivyo msafiri, au katika mvua nzito inayowapa watu uzito. Inajuzu kujumuisha kwa kutanguliza au kwa kuchelewesha, ni mamoja iwe wakati wa Dhuhr au ´Aswr, na iwe wakati wa Maghrib au ‘Ishaa.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1080/جمع-الصلاتين-في-المطر
Imechapishwa: 28/01/2026
https://firqatunnajia.com/kukusanya-swalah-kwa-sababu-ya-mvua/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket