Kukusanya mwanaume na mwanamke ndani ya kaburi moja

Swali: Je, inafaa kumkusanya mwanaume na mwanamke ndani ya kaburi moja?

Jibu: Dharurah ikipelekea kufanya hivo. Vinginevyo kila mmoja ndani ya kaburi lake. Lakini wafu wakiwa wengi na ikawa uzito kwa watu, bora ni kuweka kizuizi cha udongo kati yao [na kuweka wawili ndani ya kaburi].

Swali: Hata kama sio Mahram?

Jibu: Hata kama sio Mahram.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22638/حكم-الجمع-بين-الرجل-والمراة-في-قبر-واحد
  • Imechapishwa: 14/07/2023