Kukusanya kwa ambaye atafika anakoenda kabla ya kuingia wakati wa swalah ya pili

Swali: Kuna msafiri anajua kuwa atafika katika nchi yake kabla ya kuingia wakati wa swala ya pili. Je, inajuzu kwake kukusanya kati ya swalah mbili? Mfano wa hilo kuna mtu jua limemzamia bado akiwa safarini na akataka kuikusanya ´Ishaa wakati wa Maghrib. Je, kitendo hichi kinafaa?

Jibu: Inafaa kwa sababu bado yuko safarini. Lakini bora ni yeye kutokusanya ikiwa anafikiria au ana dhana yenye nguvu kwamba atafika katika nchi yake kabla ya kuingia wakati wa ´Ishaa au baada ya kuingia kwa wakati wake lakini bado wakati haujatoka. Hayo ni kwa sababu kukusanya ni ruhusa wakati mtu anahitajia kufanya hivo. Ni mamoja mtu yuko safarini au ni mkazi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (74) http://binothaimeen.net/content/1736
  • Imechapishwa: 25/09/2020