Kukusanya dhahabu na fedha wakati wa kutoa zakaah

Swali: Je, dhahabu na fedha hukusanywa pamoja ili kutimiza kiwango cha kutolea zakaah? Kwa mfano ukiwa na Mithaqal kumi za dhahabu pamoja na dirhamu 100 za fedha – Je, hapo inawajibika kutoa zakaah?

Jibu: Hili ndilo lililo bora zaidi, kwa sababu zote mbili zina maana moja katika hukumu ya mali. Hivyo kama zitaunganishwa ili kufikia kiwango cha kutolea zakaah – kama walivyosema baadhi ya wanazuoni – basi hilo ni jambo jema.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1079/هل-يجمع-بين-الذهب-والفضة-عند-زكاتهما
  • Imechapishwa: 15/12/2025