Swali: Njiani tunaona maovu na khaswa yale ya waziwazi kama vile sigara, wanaume wanaovaa nguo yenye kuvuka kongo mbili za miguu na mengineyo kiasi kikubwa. Je, ni wajibu kwa mtu kukataza kila uovu unaomkabili pamoja na kuwa jambo hili lina tabu kubwa?
Jibu: Uhalisia wa mambo, ni kama alivyosema muulizaji, ni jambo lisilowezekana kwa mtu kukataza kila uovu anaouona sokoni kutokana na wingi wake. Endapo atafanya hivo basi hatotembea; akipiga hatua moja au mbili atamuona mwenye kunyoa ndevu zake, atamuona mwenye kuvuta sigara, atamuona mwanamke mwenye kuvaa vibaya, atamuona mwanaume anayevaa nguo yenye kuvuka tindi mbili za miguu n.k. Kusema asimame na kila mmoja ni jambo gumu. Hili sio wajibu. Huenda akifanya hivo itakuwa ni kichekesho kwa watu. Lakini anachoweza kufanya ni kumsimamisha mtu ambaye anaona yuko karibu zaidi na kukubali katika minasaba mbalimbali na akamwambia kwa siri ya kwamba kitendo hichi anachofanya ni haramu na kwamba hakijuzu. Allaah (Ta´ala) amesema:
لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا
”Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[1]
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[2]
Ama kuhusu swali la ndugu yetu juu ya masuala ya sigara mimi naona kuwa watu wamesitisha kwa kiasi kikubwa. Ninavyodhania ni kwamba vijana hivi sasa asilimia 20% hakuna katika wao wanaovuta sigara. Hivi ni vile ninavyodhania kwa sababu sizunguki kwenye masoko. Haya ndio ninayoyaona. Kwa hali yoyote kinachotakikana ni mtu asiyazungushe mambo zaidi kuliko uhalisia.
Nashangazwa na wale wanaovuta sigara. Inadhuru mwili, inapoteza pesa, inapoteza wakati, inawaudhi viumbe, inaharibu meno, inaleta harufu mbaya n.k. Kwa msemo mwingine madhara yake ni mengi. Nimeambiwa kuwa nchi nyingi ambazo kwa mtazamo wa watu wengi wanaona kuwa zimeendelea katika mambo ya kidunia wamepiga marufuku sigara kabisa. Kwa kiasi cha kwamba endapo mmoja katika wao akilazimika kuvuta basi anaenda sehemu kuvuta kwa kujificha. Haya pamoja na kuwa ni nchi za kikafiri. Hali imefikia kiasi cha kwamba wale walioko kwenye ndege wakipita juu ya serekali kama hizi basi wanasitisha uvutaji. Watu wanavuta sigara juu angani. Ikiwa hali ndo hii ya makafiri hawa ambao hawajui kumuabudu Allaah (´Azza wa Jall) kwa Shari´ah tusemeje sisi ambao ni waislamu! Naomba Allaah uongofu kwa wote.
[1] 02:286
[2] 64:16
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (38) http://binothaimeen.net/content/867
- Imechapishwa: 18/05/2020

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (38) http://binothaimeen.net/content/867
Imechapishwa: 18/05/2020
https://firqatunnajia.com/kukemea-kila-ovu-unalokutana-nalo/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)