Swali: Ni upi wajibu wa kijana wa Kiislamu katika nyumba yake kuhusu Tv anapoingia nyumbani na akakutana muziki kwenye TV. Je, aende kwenye TV na kuifunga?

Jibu: Wajibu kwa kijana mwanaume na mwanamke na watu wote ni kukataza maovu. Hili sio jambo maalum kwa vijana. ni kwa mwanaume, mwanamke, mkubwa na mdogo. Ni wajibu kwao wote kwa kiasi cha kumcha kwao Allaah na ghera yao kwa Allaah basi wajibu wao unakuwa mkubwa zaidi. Wakijua dini ya Allaah na wakajua yale Aliyowawajibishia Allaah juu yao basi wajibu wao unazidi kuwa mkubwa. Wakikutana na mambo ya kipuuzi kwenye TV anachotakiwa ni kumpa nasaha mke wake, baba yake na ndugu zake na kuwaambia wamche Allaah. Wakiitikia, sawa, la sivyo atoke na asihudhurie pamoja nao maovu. Huu ndio wajibu kwake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=6898
  • Imechapishwa: 05/05/2015