Swali: Mtu amesafiri kutokea Riyaadh kwenda Makkah kwa kuweka nia ya kufanya ´Umrah moja. Baada ya kufanya ´Umrah akafikiria kufanya ´Umrah kwa mara ya pili. Je, inafaa kwake kufanya hivo? Afanye Ihraam kutokea wapi?

Jibu: Hakuna ubaya akifanya ´Umrah kisha akataka kufanya ´Umrah kwa niaba ya baba yake aliyekufa au mama yake au kadhalika. Atatokea kwenda Tan’iym, al-Ja’raanah au ´Arafaat na kisha baada ya hapo aingie Ihraam kwa kufanya ´Umrah mpya. Anatakiwa kutoka nje ya Haram. Kama vile ´Aaishah alivyofanya ´Umrah kwa amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokea Tan’iym.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24663/هل-يجوز-تكرار-العمرة-ومن-اين-يحرم
  • Imechapishwa: 20/11/2024