Swali: Je, inajuzu kurudia kumswaliwa maiti?

Jibu: Kama itatokea hakuna tatizo. Ikiwa tayari wameshamswalia maiti kisha akakutana na watu wengine wanaomswalia tena kaburini, naye akaswali pamoja nao, hilo halina shida wala dhambi. Ni kama mtu anayeswali swalah nyingine kwa kurudia kwa sababu ya sababu ya Kishari´ah. Mfano mtu akiswali msikitini, kisha akaenda msikiti mwingine kwa haja au kwa ajili ya darsa, akawakuta wanaswali, anaruhusiwa kuswali pamoja nao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha hivyo. Hivyo hapana vibaya kurudia swalah kwa sababu ya Kishari´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1146/حكم-تكرار-الصلاة-على-الميت
  • Imechapishwa: 31/01/2026