Kukariri Aayah mara nyingi katika Ruqyah

Swali: Kuna baadhi ya watu wanapomsomea mtu na kufikia Aayah fulani, wanaikariri mara nyingi. Kwa mfano mmoja wao kusema: “NaaruAllaahi muuqadah” kisha anaikariri kwa kirefu. Pindi tunapowakataza wanasema huku ni kumkomesha Shaytwaan. Ni lipi jibu lako?

Jibu: Sijui kama hili lina asli. Kukariri “NaaruAllaahi muuqadah” au mfano wa hayo au “´Alayhim naarun mu-uswadah”, sijui kama hili lina asli. Lililowekwa ni kuomba kinga kwa Allaah. Ikiwa kama anaogopa, anaweza kusema “A´udhibi Allaahi min sharri hadhaa” (ninajilinda kwa Allaah kutokana na shari ya huyu) baina yake yeye na Mola Wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=14579
  • Imechapishwa: 21/11/2014