Swali: Nilitembelea Ubelgiji kwenye kituo kimoja cha Kiislamu kwa ajili ya kuswali. Nikakuta wanajumuisha baina ya Maghrib na ´Ishaa´ kwa hoja ya kwamba ´Ishaa´ inachelewa kuingia na waka na inakaribia usiku wa manene na kwamba watu wanafanya kazi na wamechoka na hawawezi kusubiri. Ni ipi hukumu ya ujumuishaji huu? Inafaa kwao kufanya hivi?

Jibu: Haijuzu kwao kujumuisha kati ya Maghrib na ´Ishaa´ isipokuwa kama kunanyesha. Hili tu ndio limethibiti katika Sunnah. Haijuzu kujumuisha kwa sababu tu ´Ishaa´ inachelewa kuingia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (37) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%201%20-%2011%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017