Kujitibu kwa kitu cha haramu kutokana na haja

Swali: Ni ipi hukumu ya kujitibu kwa kitu kilichoharamishwa ikiwa kuna haja?

Jibu:

”Enyi waja wa Allaah, jitibuni, lakini msitibie kwa kitu kilichoharamishwa.”

Allaah amesema:

وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ

”… na ilihali ameshapambanua kwenu yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura.”[1]

Swali: Vipi kuhusu kujitibu kwa vitu vilivyoharamishwa?

Jibu: Ikiwa mtu atalazimika tu.

Swali: Je, pombe nayo inajumuishwa katika hali hiyo?

Jibu: Hata pombe, kama mtu ameziba koo na hakuna kingine isipokuwa hiyo, basi anaweza kumeza kiasi kinachoondoa khatari ya kufa.

Swali: Lakini inaweza kutumika kama tiba?

Jibu: Hapana, haitumiki kama tiba, isipokuwa katika dharurah ya ghafla ambayo si tiba ya kawaida, bali ni kujiokoa na mauti, mfano kutoa damu kwa mwenye kuhitaji ili kuokoa maisha.

[1] 06:119

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31639/ما-حكم-التداوي-بالمحرم-للحاجة
  • Imechapishwa: 12/11/2025