Kujionyesha kumempelekea kupata mwisho mbaya

Swali: Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)::

”Hakika mja atafanya matendo ambayo yanaonekana kwa watu kuwa ni ya watu wa Peponi… ”[1]?

Jibu: Kinachodhihiri ni kwamba mtu huyo ni mnafiki au ni mwenye kujionyesha katika matendo anayoyaonyesha. Hata kama sio mnafiki kwa ndani, lakini kule kujionyesha na kuchukulia kwake mambo wepesi kumempelekea katika kupata mwisho mbaya. Tunamwomba Allaah usalama.

[1] Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mja atafanya matendo ya watu wa Motoni mpaka kusiwe kati yake yeye na hiyo isipokuwa dhiraa akatanguliwa na kitabu ambapo akafanya matendo ya watu wa Peponi na akaingia ndani yake. Hakika mtu atafanya matendo ya watu wa Peponi mpaka kusiwe kati yake yeye na hiyo isipokuwa dhiraa akatanguliwa na kitabu ambapo akafanya matendo ya watu wa Motoni aakaingia ndani yake.” (al-Bukhaariy (3208) na Muslim (2643).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24353/معنى-العبد-ليعمل-فيما-يرى-الناس-بالحديث
  • Imechapishwa: 02/10/2024