Swali: Mtu akiswali na akaingiwa na jambo la kujionyesha katika Rak´ah moja wapo – je, mtu aseme kuwa Rak´ah hiyo pekee ndio imeharibika na ni lazima kuirudia?

Jibu: Wanazuoni wametofautiana katika hili kama kujionyesha kunaiharibu swalah kuanzia mwanzo wake au atalipwa thawabu ile sehemu ya mwanzo ya swalah na kuharibika ile sehemu yake ya mwisho? Kilichotangaa kwa wanazuoni ni kwamba kunaiharibu mwanzo na mwisho wake. Kujionyesha kunaibatilisha yote ikiwa kitendo ni chenye kuungana. Hilo ni tofauti na kitendo ambacho hakikuungana kama mfano wa kisomo cha Qur-aan na mfano wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21905/هل-الرياء-الطارى-يفسد-الصلاة
  • Imechapishwa: 01/10/2022