Kujilinda na maneno ya Allaah katika kila wakati

Swali: Ni upi usahihi wa ambaye anafupizika kujilinda na maneno ya Allaah[1] katika Adhkaar za jioni peke yake pasi na Adhkaar za asubuhi?

Jibu: Hapana, ni yenye kuenea katika kila wakati. Mtu anatakiwa kujilinda na maneno ya Allaah katika kila wakati.

[1] أَعُوْذُ بِكَلِماتِ اللَّهِ التَّامَّتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ

”Najilinda kwa maneno ya Allaah yaliyotimia kutokamana na shari Alivyoviumba.” (Atakayeyasema mara tatu jioni, basi hatodhuriwa na mdudu wa sumu usiku huo.” Ahmad (02/290), an-Nasaa´iy katika “‘Amal-ul-Yawm wal-Laylah” (590) na Ibn-us-Sunniy (68). Tazama “Swahiyh-ut-Tirmidhiy (03/187), “Swahiyh Ibn Maajah” (92/266), “Tuhfat-ul-Akhyaar”, uk. 45. )

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24545/هل-التعوذ-بكلمات-الله-في-اذكار-المساء-فقط
  • Imechapishwa: 26/10/2024