Swali: Ni muadhini yupi mtu amuitikie anaposikia muadhini mmoja baada ya mwingine?
Jibu: Awaitikie wote, kutokana na kuenea kwa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mnapomsikia muadhini, basi semeni kama anavosema muadhini.”[1]
Lakini akishaswali kisha ndio akamsikia muadhini, udhahiri wa Hadiyth ni kwamba anatakiwa pia kumuitikia. Baadhi ya wanazuoni wanasema kuwa hatoitikia, kwa sababu sio yeye mwenye kuitwa kwa adhaana hiyo. Kwa hivyo hatomrudilia. Wanaona kuwa haiwezekani akaadhini mwingine baada ya kuswaliwa kwa namna ya kwamba Hadiyth ikafanyiwa kazi kama hali ilivyokuwa katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa vile adhaana hazikuwa zikiingiliana. Lakini mwenye kuchagua kuenea kwa Hadiyth na akaitikia adhaana, yuko katika kheri.
[1] Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/193-194)
- Imechapishwa: 10/08/2026
Swali: Ni muadhini yupi mtu amuitikie anaposikia muadhini mmoja baada ya mwingine?
Jibu: Awaitikie wote, kutokana na kuenea kwa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mnapomsikia muadhini, basi semeni kama anavosema muadhini.”[1]
Lakini akishaswali kisha ndio akamsikia muadhini, udhahiri wa Hadiyth ni kwamba anatakiwa pia kumuitikia. Baadhi ya wanazuoni wanasema kuwa hatoitikia, kwa sababu sio yeye mwenye kuitwa kwa adhaana hiyo. Kwa hivyo hatomrudilia. Wanaona kuwa haiwezekani akaadhini mwingine baada ya kuswaliwa kwa namna ya kwamba Hadiyth ikafanyiwa kazi kama hali ilivyokuwa katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa vile adhaana hazikuwa zikiingiliana. Lakini mwenye kuchagua kuenea kwa Hadiyth na akaitikia adhaana, yuko katika kheri.
[1] Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/193-194)
Imechapishwa: 10/08/2026
https://firqatunnajia.com/kuitikia-adhaana-nyingi-zinazotolewa-wakati-mmoja/