Swali: Kuinama wakati wa kutoa?
Jibu: Haijuzu, hapana isipokuwa kama amekaa. Katika hali hiyo inafaa kumsogelea na kumpa salamu au kumbusu. Lakini kuinama wakati wa kutoa salamu hapana. Atoe salamu akiwa wima, kisha asalimiane kwa mikono au akumbatiane. Imepokelewa Hadiyth yenye udhaifu kuwa mtu mmoja alisema:
”Ee Mtume wa Allaah, mtu akikutana na ndugu yake amuinamie?” Akasema: ”Hapana.” Akasema: ”Amkumbatie na kumbusu?” Akasema: ”Hapana.” Akasema: ”Ashike mkono wake na asalimiane naye?” Akasema: ”Ndio.”
Kusalimiana kwa mikono ndiko kukamilika zaidi. Ikiwa watakumbatiana, kama ilivyokuja katika Hadiyth Swahiyh, hakuna tatizo katika hilo wakati wa kufika kutoka safarini. Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walipokuwa wanafika kutoka safarini wanakumbatiana. Wakikutana njiani wanapeana mikono.”
Faatwimah alikuwa akimjia baba yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasimama kumwelekea ambapo anambusu, akamshika mkono na kumketisha katika nafasi yake. Yeye pia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa akiingia kwake alikuwa akisimama kumwelekea, akimbusu na kumshika mkono wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Mkusudio ni kwamba hakuna tatizo kumbusu kichwani au kati ya macho wakati wa kuwasili kutoka safarini, kwa mama au kwa baba. Hilo halina tatizo. Kubusu na kukumbatiana kwa shingo ni bora zaidi, kama vile huyu anakumbatia shingo ya huyu na huyu anakumbatia shingo ya huyu – hiyo ndiyo inayoitwa kukumbatiana. Abu Bakr asw-Swiddiyq alikuwa akimbusu binti yake ´Aaishah shavuni alipomjia akiwa mgonjwa (Radhiya Allaahu ´anhaa).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31339/ما-حكم-الانحناء-في-التحية
- Imechapishwa: 21/10/2025
Swali: Kuinama wakati wa kutoa?
Jibu: Haijuzu, hapana isipokuwa kama amekaa. Katika hali hiyo inafaa kumsogelea na kumpa salamu au kumbusu. Lakini kuinama wakati wa kutoa salamu hapana. Atoe salamu akiwa wima, kisha asalimiane kwa mikono au akumbatiane. Imepokelewa Hadiyth yenye udhaifu kuwa mtu mmoja alisema:
”Ee Mtume wa Allaah, mtu akikutana na ndugu yake amuinamie?” Akasema: ”Hapana.” Akasema: ”Amkumbatie na kumbusu?” Akasema: ”Hapana.” Akasema: ”Ashike mkono wake na asalimiane naye?” Akasema: ”Ndio.”
Kusalimiana kwa mikono ndiko kukamilika zaidi. Ikiwa watakumbatiana, kama ilivyokuja katika Hadiyth Swahiyh, hakuna tatizo katika hilo wakati wa kufika kutoka safarini. Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walipokuwa wanafika kutoka safarini wanakumbatiana. Wakikutana njiani wanapeana mikono.”
Faatwimah alikuwa akimjia baba yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasimama kumwelekea ambapo anambusu, akamshika mkono na kumketisha katika nafasi yake. Yeye pia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa akiingia kwake alikuwa akisimama kumwelekea, akimbusu na kumshika mkono wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Mkusudio ni kwamba hakuna tatizo kumbusu kichwani au kati ya macho wakati wa kuwasili kutoka safarini, kwa mama au kwa baba. Hilo halina tatizo. Kubusu na kukumbatiana kwa shingo ni bora zaidi, kama vile huyu anakumbatia shingo ya huyu na huyu anakumbatia shingo ya huyu – hiyo ndiyo inayoitwa kukumbatiana. Abu Bakr asw-Swiddiyq alikuwa akimbusu binti yake ´Aaishah shavuni alipomjia akiwa mgonjwa (Radhiya Allaahu ´anhaa).
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31339/ما-حكم-الانحناء-في-التحية
Imechapishwa: 21/10/2025
https://firqatunnajia.com/kuinama-wakati-wa-kusalimiana/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket