Swali: Hadiyth ya pili inasema:
”Yeyote anayeapiwa kwa Allaah, basi aridhike, na asiyeridhika hatokani na Allaah.”?
Jibu: Hadiyth hii haina neno. Kwa maana nyingine ni nzuri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yeyote anayeapa kwa Allaah basi aseme kweli. Yeyote anayeapiwa kwa Allaah, basi aridhike, na asiyeridhika hatokani na Allaah.”
Hii ni katika migogoro. Pindi kiapo kinapoelekezwa kwake na mdai hana ushahidi, basi akiapa yule anayepingana naye, aridhike kwa hukumu ya Allaah. Hesabu ni siku ya Qiyaamah iwapo atakuwa amedanganya. Ikiwa atasema: ”Unayo dinari 100, 1000 au zaidi” naye hana ushahidi, basi hana jengine isipokuwa kiapo. Hivyo yule mwenye kuapa amche Allaah, na mdai aridhike kwa hukumu ya Allaah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29326/ما-صحة-حديث-من-حلف-له-بالله-فليرض
- Imechapishwa: 03/09/2025
Swali: Hadiyth ya pili inasema:
”Yeyote anayeapiwa kwa Allaah, basi aridhike, na asiyeridhika hatokani na Allaah.”?
Jibu: Hadiyth hii haina neno. Kwa maana nyingine ni nzuri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yeyote anayeapa kwa Allaah basi aseme kweli. Yeyote anayeapiwa kwa Allaah, basi aridhike, na asiyeridhika hatokani na Allaah.”
Hii ni katika migogoro. Pindi kiapo kinapoelekezwa kwake na mdai hana ushahidi, basi akiapa yule anayepingana naye, aridhike kwa hukumu ya Allaah. Hesabu ni siku ya Qiyaamah iwapo atakuwa amedanganya. Ikiwa atasema: ”Unayo dinari 100, 1000 au zaidi” naye hana ushahidi, basi hana jengine isipokuwa kiapo. Hivyo yule mwenye kuapa amche Allaah, na mdai aridhike kwa hukumu ya Allaah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29326/ما-صحة-حديث-من-حلف-له-بالله-فليرض
Imechapishwa: 03/09/2025
https://firqatunnajia.com/kuheshimu-kiapo-cha-allaah-2/