Kuhamisha damu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwengine

Swali: Ni ipi hukumu ya kuhamisha damu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine? Ikisemwa kuwa inajuzu, je, yule anayechukuliwa damu anaingia dhambini akipata madhara au akafariki kwa sababu hiyo? Je, hilo linaingia katika onyo la yule aliyejiua mwenyewe?

Jibu: Kuhamisha damu kutoka kwa mtu kwenda kwa mwingine kuna ufafanuzi. Ikiwa kuna dharurah na kuhamisha damu hakumdhuru anayetoa damu, basi hakuna tatizo kwa mujibu wa maoni sahihi, kwa sababu ya dharurah. Hapo khaswa ikiwa madaktari waliobobea wanasema kuwa kiasi hicho cha damu hakimdhuru na kwamba yule mwenye kuhitaji damu yuko katika dharurah na damu hiyo inalingana na damu yake, basi hakuna tatizo katika hilo –  kwa idhini ya Allaah – kwa mujibu wa maoni yaliyochaguliwa. Lakini ikiwa kuhamisha damu kunamdhuru anayetoa damu, basi haifai. Kwani hairuhusiwi mtu kujidhuru kwa ajili ya maslahi ya mwingine. Lakini ikiwa daktari bingwa na mwenye ujuzi atathibitisha kuwa kiasi hicho cha damu hakimdhuru mtu huyo na yule mwingine anakihitaji, basi hakuna tatizo kufanya hivyo kwa mlango wa kujitolea na kwa mlango wa kufanya wema.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1414/حكم-نقل-الدم-من-شخص-الى-اخر
  • Imechapishwa: 13/12/2025